Exodus 35:10-15

10 a“Wote wenye ujuzi miongoni mwenu inawapasa kuja na kutengeneza kila kitu Bwana alichoamuru: 11 bMaskani pamoja na hema lake na kifuniko chake, vibanio, mihimili, mataruma, nguzo na vitako; 12 cSanduku la Agano pamoja na mipiko yake, kifuniko cha kiti cha rehema na pazia linalokizuia; 13 dmeza na mipiko yake pamoja na vyombo vyake vyote, mikate ya Wonyesho; 14 ekinara cha taa kwa ajili ya mwanga pamoja na vifaa vyake vyote, taa na mafuta kwa ajili ya mwanga; 15 fmadhabahu ya kufukiza uvumba pamoja na mipiko yake, mafuta ya upako na uvumba wenye harufu nzuri; pazia la mlangoni mahali pa kuingilia ndani ya maskani;
Copyright information for SwhKC